Uncategorized

MCHEZO MZIMA WA CHAMA KUREJEA BONGO UNACHORWA NAMNA HII

admin May 27, 2020 7:47 am


CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba yupo kwenye mchakato wa kurejea nchini ili kuungana na wachezaji wenzake ambao wameingia kambini leo maeneo ya Mbweni.

Habari zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Simba umeanza mawasiliano na uongozi wa Serikali ya Zambia ili kujua namna ya kuweza kumpata nyota huyo kupitia Wizara ya Habari ya nchini Zambia.

“Tayari uongozi wa Simba umeanza mawasiliano na uongozi wa Serikali ya Zambia kupitia Wizara ya michezo ili kujua namna itakayofaa kumpata Chama, inawezekana na mambo yatakuwa sawa,” ailieleza taarifa hiyo.

Jana, Meddie Kagere raia wa Rwanda aliwasili nchini na leo anatarajia kujiunga na wenzake ambao wapo kambini kuanza mazoezi.

Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa mpango wa kuwarejesha wachezaji upo na kila kitu kikiwa sawa mambo yatawekwa hadharani. 

VIDEO:MREMBO WA BURUNDI ANAYEKIPIGA SIMBA QUEENS YEYE NI MWENDO WA NYUNGU KIMMCHI AZIMA NDOTO ZA DORTMUND KUSEPA NA POINTI TATU MAZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply