Morice Chukwu
Yanga SC

Morice Chukwu Alipwa Bilioni 4.02 Lebanon, Aicha Yanga Mdomo Wazi

Vardo August 18, 2026 9:36 am

Kiungo wa zamani wa Singida Black Stars, Morice Chukwu, amekamilisha usajili wa maajabu kwenda klabu ya Jwaya SC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Lebanon kwa mkataba wa miaka miwili, uhamisho uliompa jeuri kubwa ya kifedha.

Chukwu, ambaye kwa muda mrefu alikuwa akihusishwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga SC, ametimkia Lebanon baada ya kuwekewa mezani kitita kinachokadiriwa kufikia Sh1.8 bilioni kama ada ya usajili (sign-on fee) akiwa mchezaji huru.

Mbali na ada hiyo ya usajili, kiungo huyo aliyekuwa na msimu bora atakuwa akipokea mshahara wa Sh90 milioni kila mwezi. Hesabu za mshahara pekee zinamfanya kuvuna Sh1.08 bilioni kwa mwaka, na kufikisha jumla ya Sh2.16 bilioni ndani ya miaka miwili ya mkataba wake. Ukijumlisha na ada ya usajili, Chukwu anaondoka na kitita cha zaidi ya Sh4.02 bilioni.

Chanzo cha karibu na mchezaji huyo kimeeleza:

“Chukwu alikuwa na chaguo kadhaa baada ya kumaliza mkataba wake na Singida Black Stars, lakini Jwaya SC walikuja na ofa kubwa ambayo haikuwa rahisi kuikataa. Yanga walimtafuta mwanzoni kuangalia uwezekano wa kumpata lakini hawakurudi tena mara ya pili, ndipo akaamua kuchukua fursa hii ya Lebanon.”

Dili hili limekamilika Agosti 15, 2026, mara baada ya mkataba wake na Singida Black Stars kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2025-2026.

Takwimu za Morice Chukwu:

  • Msimu wa 2025-2026 (Singida Black Stars): Alicheza mechi 17 za Ligi Kuu Bara na mechi 5 za Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

  • Uzoefu wa Afrika: Alicheza mechi 147 Ligi Kuu ya Nigeria (NPFL) na kufunga mabao 6.

  • Mashindano ya CAF: Mechi 22 za Kombe la Shirikisho (mbao 1) na mechi 6 za Ligi ya Mabingwa Afrika.

  • Mataji: Bingwa mara mbili wa NPFL akiwa na Akwa United (2020-2021) na Rivers United (2021-2022).

Uhamisho huu unamfanya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 kuanza ukurasa mpya katika soka la Kimataifa huku akiongeza uzoefu mkubwa kwenye taaluma yake.

Rekodi Zawabeba Mashujaa, Namungo Ligi Kuu Bara Leo Coastal Union Yainasa Saini ya Ahmed Issa Mbele ya Simba SC