Rumor za Usajili Ulaya: Parrott, Endrick, Van Dijk na McTominay
Ligi Kuu na masoko ya usajili barani Ulaya yanaendelea kushika kasi huku klabu mbalimbali zikiendelea kupanga safu zao kuelekea dirisha dogo la usajili la Januari na lile kubwa la kiangazi. Hazi hapa taarifa za hivi karibuni za usajili kutoka kwenye klabu kubwa Ulaya:
Real Betis Yaweka Ngumu Kwa Troy Parrott Klabu ya Real Betis haina hofu kuhusu uwezekano wa kumpoteza mshambuliaji wake hatari, Troy Parrott. Klabu ya Tottenham Hotspur, ambayo ni waajiri wake wa zamani, italazimika kutoa kitita cha Dola 112.5 milioni ili kufanikisha kifungu cha kuvunja mkataba wake (buyout clause). Parrott, ambaye alianzia akademi ya Spurs kabla ya kutimkia AZ Alkmaar na kisha Betis, amekuwa kwenye kiwango bora kilichovutia pia timu kama Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid.
Bournemouth Yamchunga Alex Scott Bournemouth haina mpango wa kumruhusu kiungo kijana Alex Scott kuondoka mwezi Januari licha ya Chelsea na Liverpool kuonyesha nia ya kumsajili. Hata hivyo, klabu hiyo tayari imeanza kumfuatilia kiungo wa Wolverhampton Wanderers, Fer Lopez, kama mbadala iwapo itashindwa kumzuia Scott.
Virgil van Dijk Kubaki Liverpool? Beki na nahodha wa Uholanzi, Virgil van Dijk, yupo kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Liverpool. Hii inajiri baada ya kumshawishi kocha Andoni Iraola kuhusu mchango wake kikosini, licha ya awali kuwepo kwa ripoti kuwa kocha huyo alitaka kuachana naye mwanzoni mwa mwaka mpya.
Scott McTominay Kurejea Premier League Kiungo wa Napoli, Scott McTominay, anatarajiwa kuondoka nchini Italia na kurejea Ligi Kuu England (EPL) msimu ujao wa kiangazi. Mazungumzo ya mkataba mpya na Napoli yamesimama, huku klabu zake za zamani ikiwemo Manchester United pamoja na Aston Villa zikipambana kupata saini yake.
Vangelis Pavlidis Aendelea Kuota Ndoto Za EPL Licha ya kuwekewa ngumu na klabu yake ya Benfica, mshambuliaji Vangelis Pavlidis bado ana nia ya kujiunga na timu ya Ligi Kuu England. Mchezaji huyo anawaniwa kwa karibu na klabu za Aston Villa na Tottenham Hotspur.
Vita Ya Luka Vuskovic Manchester United, Liverpool na Real Madrid zote zipp kwenye vita ya chini kwa chini kuwania saini ya beki wa kati wa Brighton, Luka Vuskovic. Hata hivyo, Brighton imeweka wazi kuwa haitakuwa tayari kumuuza wakati wa dirisha dogo la Januari bali mwishoni mwa msimu.
Arsenal Yaitazama Saini Ya Breno Bidon Kiungo chipukizi Mbrazili, Breno Bidon (21) anayechezea Corinthians, yupo kwenye rada za Arsenal. Washika Bunduki hao wa London wapo tayari kulipa kiasi cha Dola 28 milioni kilichopo kwenye mkataba wake ili kuvunja mkataba na kukamilisha usajili huo.
Liverpool Yafikiria Kumpiga Chini Mamardashvili Klabu ya Liverpool ipo tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya golikipa Giorgi Mamardashvili. Viongozi wa klabu hiyo wana shaka kama kipa huyo aliyesajiliwa kutoka Valencia ana uwezo wa kuwa mrithi wa muda mrefu wa Alisson Becker.
Joao Felix Na Dani Olmo Mambo Yachanganya Barcelona inavutiwa na mpango wa kumrejesha mshambuliaji Joao Felix kutoka Al Nassr mwezi Januari. Hata hivyo, ujio wa Felix unaweza kusababisha kuondoka kwa Dani Olmo ambaye anawaniwa kwa karibu na Bayern Munich.
Real Madrid Yatoa Msimamo Wa Endrick Licha ya Arsenal na Tottenham Hotspur kutaka huduma ya mshambuliaji chipukizi Endrick, Real Madrid imesisitiza kuwa haitawaza kumuuza mazima mwezi Januari. Badala yake, mabingwa hao wa Ulaya wapo tayari kumtoa kwa mkopo wa miezi sita pekee ili apate muda mwingi wa kucheza kabla ya kurejea kikosini.