Ligi Kuu Zanzibar
Michezo Bongo

Zimamoto na Polisi Zazidi Kutikisa Ligi Kuu Zanzibar | Msimamo wa ZPL

Vardo October 6, 2026 6:43 pm

Timu za Zimamoto na Polisi Zanzibar zimeendelea kuonyesha ubora na makali ya hali ya juu katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuweka rekodi ya kuwa klabu pekee ambazo hazijala ladha ya kipigo hadi sasa.

Kati ya timu 16 zinazochuana vikali katika ligi hiyo, miamba hiyo miwili imezicheza mechi sita bila kupoteza hata moja.

Zimamoto Yaikamata Kilele cha ZPL

Zimamoto ipo kileleni mwa msimamo wa ZPL ikiwa na pointi 16. Katika mechi zake sita, imeshinda michezo mitano dhidi ya:

  • Muembe Makumbi

  • Chipukizi

  • Mafunzo

  • Wembe

  • KMKM

Sare yao pekee ilikuwa dhidi ya Polisi Zanzibar.

Polisi Yagandamia Nafasi ya Tatu

Kwa upande wa Polisi Zanzibar, wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 12. Wameshinda mechi tatu dhidi ya KVZ, Fufuni, na Mlandege, huku wakitoka sare kwenye michezo mitatu dhidi ya Mwenge, Mafunzo, na Zimamoto.

JKU Yaistua Uhamiaji FC

Uhamiaji FC, ambayo awali ilikuwa kinara na haijapoteza mechi, ilipokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa JKU. Matokeo hayo yaliwashusha hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 15 (ushindi mechi 5 na kipigo 1).

Hali Mbaya Kwa Fufuni na Mafunzo

Wakati Zimamoto na Polisi zikisherehekea matokeo mazuri, mambo ni magumu kwa Fufuni FC na Mafunzo FC ambazo hazijapata ushindi wowote baada ya mechi sita:

  • Fufuni FC: Inaburuza mkia ikiwa na pointi 2 pekee (sare 2, vipigo 4). Ndiyo timu iliyochukua mabao mengi zaidi (10) huku ikifunga 3 pekee.

  • Mafunzo FC: Inakamata nafasi ya 13 ikiwa na pointi 4 zilizotokana na sare 4 na vipigo 2.

Kila Spin Ni Safari Ya Dhabu! Shindania Tzs 4,000,000 Daddy Francis Afichua Mfumo Unavyoibeba Vibaya Chipukizi ZPL