Uncategorized

WACHEZAJI SIMBA WAFANYIWA VIPIMO

admin May 27, 2020 9:47 am


WACHEZAJI wa Simba leo baada ya kuwasili kambini wamefanyiwa vipimo vya afya ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kuelekea maandalizi ya kumaliza mechi za mzunguko wa pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa wapo kambini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

‘Tumeshawasili kambini na wachezaji wameanza kuripoti, kikubwa ambacho kinafanyika ni kuanza kuwafanyia vipimo ili kujua afya zao kisha program nyingine zitafuata,”

Miongoni mwa wachezaji ambao wamewasili kambini leo ni pamoja na nahodha msaidizi Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Beno Kakolanya na Said Ndemla.

KOCHA AIBUKA NA KUSEMA ANAIDAI YANGA WADADA NI ANA BALAA NDANI YA UWANJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply