Mahammadou Kasali Simba SC
Michezo Bongo

Kipa Mahammadou Kasali Kurejea Uwanjani Hivi Karibuni!

Vardo August 19, 2026 1:05 pm

Mambo yanaendelea kuwa mazuri ndani ya kikosi cha Simba SC baada ya kipa wao namba moja, Mahammadou Kasali, kupiga hatua kubwa katika uuguzaji wa jeraha lake la goti na kutarajiwa kurejea uwanjani hivi karibuni.

Kasali alipata jeraha hilo katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu wa 2026/27 dhidi ya Kagera Sugar, uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, na kulazimika kufanyiwa mabadiliko ya mapema.

Akizungumzia maendeleo ya kipa huyo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa hali ya Kasali inaendelea vizuri sana na yuko mbioni kujiunga na wenzake mazoezini.

Licha ya kukosa mchezo wa leo dhidi ya Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Steve Barker lina matumaini makubwa ya kumtumia mchezaji huyo katika mechi zinazofuata.

“Tutakosa huduma ya Kasali katika mchezo wetu wa leo, lakini tunatarajia katika mechi zijazo atakuwa sehemu ya kikosi kutokana na maendeleo yake kuwa mazuri sana,” alisema Ahmed Ally.

Kurejea kwa Kasali ni habari njema na pigo la furaha kwa benchi la ufundi na mashabiki wa Msimbazi, kwani kipa huyo amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Simba SC.

Steve Barker Aitahadharisha Simba SC Akimkosa Kipa Mahamadou Kasali Dhidi ya Pamba Jiji Kocha Yanga Afunguka Sababu ya Kumweka Nje Stephane Aziz Ki