Uncategorized

NAMUNGO:TUMEUKUMBUKA MPIRA

admin May 31, 2020 3:47 am


ADAM Oseja, mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha Namungo FC kilicho chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery amesema kuwa anafurahia kurejea kwa mechi za ushindani kwa kuwa walikuwa wameukumbuka mpira.

Shughuli za michezo zilisimamishwa tangu Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ila kwa sasa Serikali imesema kuwa mambo yanaweza kuendelea huku tahadhari ikichukuliwa kuanzia Juni Mosi.

Bodi ya Ligi Ligi Tanzania iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kuwa masuala ya michezo yataanza Juni 13,2020.

Akizungumza na Saleh Jembe, Oseja amesema kuwa muda mrefu walikaa bila kucheza mechi za ushindani jambo lililowafanya waukumbuke mpira. “Tulikaa muda mrefu bila kucheza ila sababu kubwa ilikuwa ni janga la Virusi vya Corona hatukuwa na namna ya kufanya, kwa kuwa mambo yanarejea tumefurahi tuliukumbuka mpira,” amesema.

ALLIANCE FC WAIPIGIA HESABU NDEFU NAMUNGO LIVERPOOL YAINGIA ANGA ZA ADAMA, MWILI JUMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply