Uncategorized

YANGA: TUPO MIKONO SALAMA HATUJAKOSEA NJIA

admin May 31, 2020 6:47 pm


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchakato wao wa mabadiliko ni ndoto yao ya muda mrefu hivyo wanaamini kwamba itafanikiwa bila mashaka yoyote yale kwa kuwa inasimamiwa na watu sahihi.

Yanga leo inaendelea safari ya mabadiliko ambapo ipo kwenye mchakato wa kutiliana saini na Kampuni ya La Liga ya Hispania pamoja na GSM.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mfumo ambao wanaufuata ni njia sahihi kufikia mafanikio yalipo.

“Tupo sahihi na tunajua kile ambacho tunakifanya kikubwa tu mashabiki wawe pamoja nasi watupe sapoti katika kile ambacho tunakifanya kwani hatujakosea njia tupo mikono ya watu salama,” amesema.

Tukio hilo la makubaliano linarushwa leo moja kwa moja kutoka Serena Hotel kupitia Azam TV na Yanga TV.

MASHINE ILIYOINGIA SIMBA YAAHIDI UBINGWA,YANGA KUMEPAMBA MOTO, KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU SIMBA YATAJA SABABU YA MECHI ZAO 10 KUWA NGUMU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply