Uncategorized

POLISI TANZANIA WAKIWA KAZINI BADO WANATAMBUA UWEPO WA CORONA

admin May 28, 2020 5:47 am


TIMU ya Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini inaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Polisi Tanzania tayari imeanza mazoezi yake kujiaanda na mechi za kumaliza msimu wa 2019/20.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa wameanza mazoezi ili kujiaandaa mapema huku wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

“Bado tunaendelea kufuata utaratibu uliowekwa na Wizara ya Afya pamoja na Serikali katika kujilinda na Corona na tumeanza mazoezi mapema ili kujiweka sawa kwani ushindani sio mchezo,”.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza ifikapo Juni Mosi.

NGWAIR ALAMA INAYOISHI BONGO YANGA YAJIPA NAFASI YA KUSHIRIKI MICHUANO YA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply