Uncategorized

CIOABA WA AZAM FC ATINGA BONGO KIBABE

admin June 1, 2020 7:47 pm

ARISTICA Cioaba,Kocha Mkuu wa Azam FC leo amewasili nchini Tanzania akitoka Romania alikokuwa kwa ajili ya mapumziko yalitokana na kuibuka kwa janga la Virusi vya Corona.

 Machi 17 shughuli za kimichezo zilisimamishwa na Serikali na zinatarajiwa kuanza Juni 13 baada ya Serikali kuridhia masuala ya michezo kurejea baada ya kueleza kuwa maambukizi yamepungua.

Cioaba amerejea na Kocha wa Viungo, Costel Birsan, wakitokea mjini Frankfurt, Ujerumani walipopata usafiri wa ndege wa kuja Tanzania.

Wawili hao wataanza kesho Jumanne jioni, kukinoa kikosi cha timu hiyo, ambacho tayari kilikuwa kimeanza mazoezi  Mei 27 chini ya Kocha Msaidizi, Bahati Vivier.

HII HAPA RATIBA YA MECHI 10 ZA SIMBA ZILIZOBAKI IBRAHIM AJIBU FRESH NDANI YA SIMBA,AANZA MAZOEZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply