Uncategorized

MBAPPE BWANA ALIWAHI KUOKOA PENALTI NJE YA 18

admin June 2, 2020 4:47 am


KYLIAN Mbappe, mshambuliaji namba moja ndani ya PSG mwenye ushikaji wa karibu na Neymar Jr, alifanya tukio ambalo watu hawakuamini macho yao kama angekuwa sahihi.

Wakati huo PSG ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Saint Etienne kwenye Ligue 1, wenyeji walipata penalti dakika ya 30 ambayo ilimfanya Mbappe afanye maajabu kwa kuokoa penalti hiyo kwa ishara akiwa nje ya 18.

Mbappe alitumia kidole cha mkono wa kushoto kumuonyesha kipa wake, Alphonse Areolo upande wa kulia wa goli lake hivyo asifanye makosa kuinasa.

Kweli bwana, mpigaji Remy Cabella alipiga upande uleule kipa akaucheza ngoma ikawa imeokolewa kimtindo na Mbappe nje ya 18.

HIVI NDIVYO WACHEZAJI YANGA WALIVYOMKOSESHA MKWASA LAKI MBILI NA TISINI DUH! SALAH KWA MASHUTI YALILONGA LANGO ANAKIMBIZA KWELI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply