Uncategorized

MBELEGIJI WA YANGA INAELEZWA KUWA HAJATUMIWA TIKETI KURUDI BONGO

admin June 2, 2020 2:47 pm


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anawasiliana na Kocha msaidizi, Boniface Mkwasa ambaye anasimamia timu kwa sasa jambo ambalo halimfurahishi kwa kuwa hajatumiwa tiketi.

Eymael aliibukia Ubelgiji baada ya masuala ya michezo kusimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.


Kwa sasa shughuli za michezo zimeruhusiwa na Serikali ambapo Mei 27 wachezaji wa Yanga waliripoti kambini na kuanza mazoezi kujiandaa na mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.


 “Mpaka sasa sijatumiwa tiketi huku muda ukiwa unazidi kwenda na tayari ratiba imeshatoka na bado sijajua hatma yangu kwani tayari anga la ndege limefunguliwa na baadhi ya ndege zimeanza kuingia,” amesema.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga,Hassan Bumbuli kwa njia ya simu ili kueleza taarifa hiyo kwa njia ya simu hakuweza kupokea.

SIMBA KWA SASA HAIPO TAYARI KUONA WACHEZAJI WAKIANZA LIGI, SABABU HII HAPA WERNER AZIINGIZA VITANI TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND NA BUNDESLIGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply