ARSENAL imeanza mchakato wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wao namba moja Pierre Emerick Aubameyang ili kumuongezea mkataba mpya ndani ya kikosi hicho.
Mkataba wa Aubameyang unameguka mwishoni mwa msimu ujao na hakujawa na mazungumzo yoyote kuhusu yeye kubaki ama kuondoka ndani ya timu hiyo na Arsenal haitaki kumuuza kwa sasa licha ya kuwa iwapo hatasaini dili jipya anaweza kuondoka bure.
Majukumu ya kumshawishi nyota huyo abaki ndani ya kikosi hicho amekabidhiwa Kocha Mkuu, Mikel Arteta aanze kumshawishi abaki ndani ya kikosi hicho kwa mujibu wa The Telegraph.
Arteta anaamini kwamba, Aubameyang anaweza kuendelea kuwa chaguo la kwanza ndani ya Arsenal hata msimu wa 2021 hivyo anahitaji kukaa chini kuzungumza naye kuhusu dili lake jipya.
Aubameyang ametupia jumla ya mabao 61 akiwa amecheza jumla ya mechi 97 baada ya kujiunga na timu hiyo Januari 2018 akitokea Dortmund.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.