Uncategorized

YANGA KUTESTI MITAMBO KWA KMC, JUNI 7

admin June 3, 2020 1:47 pm


JUNI 7 Yanga itashuka uwanja wa uhuru kukipiga dhidi ya KMC majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa timu hizo baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo kuanza baada ya kusimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza kwa kueleza kuwa maambukizi yamepungua.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa, Kocha Msaidizi, Charles Mkwassa ameomba mechi hiyo ili kujua ubora wa wachezaji wake.

“Kocha amemba apewe mechi ili kujua ubora wa kikosi chake kwani tunarejea kwenye mechi za ushindani hivyo ni muhimu kuona namna gani kikosi kitakuwa imara,” amesema.

Juni 13,Yanga itamenyana na Mwadui FC mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kambarage,Shinyanga.

VIDEO: SIMBA KUANZIA PALE WALIPOISHIA MTIBWA SUGAR INA MKAKATI WA KUJENGA BONGE MOJA YA UWANJA, HAYA HAPA MAFANIKIO YAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply