Ahmed Ally Simba
Simba SC

Ahmed Allyatoa Onyo Kali Simba SC: “Hatuna Nafasi ya Kufanya Makosa”

Vardo October 26, 2026 9:56 pm

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amewataka wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kutoridhika na uongozi wa pointi tano kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Amesisitiza kuwa kikosi kinapaswa kuongeza juhudi, umakini mkubwa, na mshikamano katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

Akizungumza kuelekea michezo ijayo baada ya kupisha michuano ya kimataifa, Ahmed alisema kuwa kila mchezo uliosalia ni mgumu na wa mwisho, hivyo hakuna nafasi ya kulegeza kamba. Simba sasa inatupa nguvu zake zote katika mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Oktoba 29 katika Uwanja wa Kwaraa, Babati.

Vile vile, ametoa wito kwa Wanamsimbazi kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti ili kuendeleza wimbi la ushindi.

“Pengo la pointi tano kwenye msimamo wa ligi lituongezee nguvu, hasira na umakini wa kupambana zaidi. Msimu huu hatuna nafasi ya kufanya makosa,” alisema Ahmed.

Msimamo huo unaonyesha wazi nia ya wekundu hao wa Msimbazi ya kutobweteka na matokeo ya sasa, bali kuifanya kuwa motisha ya kusaka ushindi ugenini Babati ili kujiweka pazuri kwenye kuwania taji la Ligi Kuu ya NBC.

Kikosi Cha Yanga Chaleta Hasira: Simon Dladla Atoa Ahadi Nzito Dhidi ya Mashujaa FC!