Simba SC Haihofii Mtu CAF! Mangungu Atuma Onyo Kali Ligi ya Mabingwa
Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, amewatoa hofu mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa kusisitiza kuwa kikosi hicho hakimhofii mpinzani yeyote katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiongeza kuwa kipaumbele chao kwa sasa ni kufanya maandalizi ya kina.
Akizungumza hivi karibuni, Mangungu alieleza kuwa Simba inasubiri kukamilika kwa mechi zote za hatua za awali za mashindano hayo ili kufahamu timu kamili zitakazoingia hatua ya makundi na kupata mwanga wa wapinzani wao watakaokutana nao.
Amesema kuwa kama klabu kongwe na kigogo wa soka barani Afrika, Simba haina sababu ya kuingia kwenye michuano hiyo ikiwa na hofu, bali inapaswa kujipanga kwa nguvu zote ili kufikia malengo yake makubwa.
“Simba ni kigogo kikubwa Afrika. Kama unaona kuna vigogo ambavyo havipo, basi Simba ipo katika michuano hiyo. Tunaenda kucheza na kushindana na timu yoyote, hatuwezi kumhofia mpinzani ambaye tutakutana naye,” amesema Mangungu.
Pamoja na kuonyesha kiwango bora kwa sasa na kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi unawatambua vyema ushindani na matokeo yasiyotabirika kwenye soka, hivyo hauwategemei mafanikio ya sasa pekee.
Alitolea mfano timu kama Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kuonyesha kuwa hakuna matokeo ya uhakika kwenye soka la kisasa, akisisitiza umuhimu wa kumpa kila mpinzani heshima inayostahili na kujiandaa kwa umakini mkubwa bila kuwadharau.