Home Uncategorized YANGA WATAJA SABABU YA KUCHAPWA MABAO 3-0 NA KMC

YANGA WATAJA SABABU YA KUCHAPWA MABAO 3-0 NA KMC


CHARLES Mkwassa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kichapo cha mabao 3-0 mbele ya KMC jana umetokana na makosa yao wenyewe waliyoyafanya ndani ya uwanja.

Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa Uwanja Uhuru na ulikuwa na ushindani mkubwa tangu mwanzo wa kipindi mpaka dakika 90 zilipokamilika.

KMC iliweza kuandika mabao yake matatu  kupitia kwa Sadala Lipangile dakika ya 31, Charles Ilanfya dakika ya 45 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Hassan Kabunda dakika ya 65.

Mkwassa amesema kuwa mbali na makosa madogo ambayo wameyafanya uwanjani pia hawakuwa na muda mrefu wa kuandaa kikosi katika mechi za ushindani kutokana na ligi kusimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

“Hatukuwa na muda mrefu wa maandalizi kwa ajili ya kikosi chetu ndio maana imekuwa rahisi kufungwa licha ya makosa ya kiufundi ambayo tumeyafanya.

“Kwa sasa tutayafanyia kazi makosa ambayo tumeyafanya kwa ajili ya kufanya vizuri mechi zetu za ligi kwani tuna mchezo dhidi ya Mwadui FC, nina amini utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana,” amesema.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA COASTAL UNION, MKWAKWANI TANGA