Home Uncategorized JEMBE LA KAZI LIMERUDI MAZIMA YANGA

JEMBE LA KAZI LIMERUDI MAZIMA YANGA


PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amerejea mazoezini baada ya kukaa nje kwa muda akiuguza majeraha yake aliyoyapata wakati wa mazoezi ya hivi karibuni.

Yanga ilianza mazoezi Mei 27 kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria ikiwa ni maandalizi ya kujiweka fiti kwa ajili ya kuendelea na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Katika maandalizi yake Yanga ilicheza mechi tatu za kirafiki ambazo zote Tshishimbi alizikosa kutokana na kuwa na majeraha.

Mechi hizo ilikuwa dhidi ya Transit Camp ambapo Yanga ilishinda mabao 3-1, Dar City hizi zote mbili zilichezwa Uwanja wa Chuo cha Sheria, Yanga ilishinda mabao 2-0 na KMC ambapo Yanga ilipoteza kwa kuchapwa mabao 3-0 Uwanja wa Uhuru.

SOMA NA HII  KAMA KAWA YANI...MORRISON KAIPIGA CHENGA YA MWILI YANGA...MASTAA WENGINE HAWA HAPA...