Uncategorized

KUMEKUCHA, MOLINGA, MAKAME NA SIBOMANA KUKATWA MSHAHARA YANGA

admin June 10, 2020 11:47 am

JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga, amesema kuwa Kocha Mkuu, Luc Eymael aliwaambia wachezaji kwamba atakayeongezeka uzito atakatwa mshahara wake ikiwa ni sehemu ya adhabu.
Abdul amesema kuwa Eymael aliwapa programu maalumu za kufanya kwa ajili ya kulinda vipaji vyao wakati wa mapumziko yaliyosababishwa na janga la Corona na kutoa onyo kwa wachezaji wote.

“Kocha alisema kuwa mchezaji ambaye ataongezeka uzito, huyo lazima atakatwa mshahara, ninaamini atakapopewa ripoti kazi ya kwanza itakuwa ni kutazama wale ambao wameshindwa kutimiza vigezo vyake,” alisema Abdul.

Inaelezwa kuwa walioongezeka uzito ambao panga la mshahara linawasubiri ni pamoja na David Molinga, Patrick Sibomana na Abdulaziz Makame
COASTAL UNION: NAMUNGO SIO TIMU NYEPESI,TUPO TAYARI KUPAMBANA LIVE: ALIKIBA AFUNGUKA CHEED NA KILLY KUONDOKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply