Uncategorized

PICHA LA MBELGIJI WA YANGA KUTUA BONGO LILIKUWA NAMNA HII

admin June 10, 2020 4:47 pm


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga leo ametua nchini Tanzania akitokea nchini Ubelgiji alikokuwa kwa ajili ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na Virusi vya Corona.

Eymael ametua Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na baadhi ya Waandishi wa Habari ambao walikuwepo hapo.

Licha ya taarifa zake za kurejea leo kuwa wazi hakukuwa na mwakilishi yoyote wa Yanga ambaye alikuwa alikuwepo uwanjani hapo.

Kocha huyo anatarajiwa kuungana na wachezaji wake kesho, Shinyanga ambao wamekwenda huko kujiandaa na mchezo dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Juni 13.


Habari zinaeleza kuwa majukumu yalikuwa mengi kwa viongozi wa Yanga siku ya leo.

“Kuna mmoja amepewa likizo na wengine wapo na timu kwenye msafara hivyo kesho mambo yatakuwa sawa,” ilieleza taarifa hiyo.

JESHI LA KMC LEO DHIDI YA AZAM FC, MCHEZO WA KIRAFIKI KILICHOMKUTA EYMAEL WA YANGA AIRPORT HIKI HAPA,BEI YA MO KUSAJILI VIUNGO, NI NDANI YA SPOTI XTRA, ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply