Uncategorized

EYMAEL AUNGANA NA YANGA KAMBINI, KESHO KAZI KUANZA MBELE YA MWADUI FC

admin June 12, 2020 6:47 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael leo amewasili kambini Shinyanga na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo ambao walitangulia Juni 10.

Eymael alichelewa kujiunga na timu ambayo ilianza mazoezi tangu Mei 27 kwa kuwa alikuwa nchini Ubelgiji ambapo anga la ndege lilifungwa kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Yanga kesho itashuka uwanja wa Kambarage kumenyana na Klabu ya Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi.

Eymael aliungana na wachezaji mazoezini ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwenye mchezo huo wa kesho, Juni 13.

MOLINGA AIBUA MAPYA NDANI YA YANGA,HUKO MSIMBAZI KUMEKUCHA, KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI MWADUI FC YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply