Uncategorized

MWADUI FC YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

admin June 12, 2020 6:47 pm


UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.

Mwadui FC itawakaribisha Yanga Uwanja wa Kambarage majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, meneja wa timu, David Chakala amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wana imani ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao.

“Tupo sawa na kila mchezaji yupo vizuri kuona kwamba timu inapata ushindi, kikubwa ni sapoti kutoka kwa mashabiki kwani timu haipo nafasi nzuri.

“Lengo letu ni kuona tunapata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kubaki ndani ya ligi, pointi tatu za Yanga ni muhimu kwetu” amesema. 

EYMAEL AUNGANA NA YANGA KAMBINI, KESHO KAZI KUANZA MBELE YA MWADUI FC SHINDA GARI SASA YAFIKA PATAMU, MSHINDI NJIANI KUPATIKANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply