Uncategorized

AZAM FC YAPIGA MTU 4G

admin June 14, 2020 6:47 pm


TIMU ya wafanyakazi wa Azam FC imefanya kweli baada ya kuwafunza soka wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwanyuka mabao 4-0.

Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Wafanyakazi wa Azam FC walionyesha umwamba mkubwa wa kutandaza soka kwa dakika zote 90 za mchezo huo.

Mabao yaliwekwa kimiani na John Matambara, aliyefunga mabao mawili huku Victor Ndozero na Feisal wakitupia mojamoja.

Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya wafanyakazi wa Azam FC, tokea timu hiyo iundwe, na mafanikio yamekuwa makubwa sana.

Timu hiyo inatoa fursa kwa timu nyingine kuomba mechi ya kirafiki ili kuonyesha burudani.

SIMBA YAKIONA CHA MOTO LEO TAIFA, YAAMBULIA POINTI MOJA MBELE YA WAZEE WA KUPAPASA KISA KUGAWANA POINTI MOJA NA RUVU, SIMBA WATOA TAMKO HILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply