INAELEZWA kuwa msimu ujao Klabu ya Namungo itakuwa na kazi ya kusuka kikosi chake upya kutokana na mitambo yake mitatu ya kazi kwa sasa kuwekwa kwenye rada za vigogo wa Dar.
Lukas Kikoti mwenye mabao manne, Bigirimana Blaise mwenye mabao 10 na Relliants Lusajo mwenye mabao 11 wamehusika kwenye mabao 25 kati ya 36 yaliyofungwa.
Lusajo na Blaise inaelezwa kuwa wapo kwenye hesabu za Yanga, huku Kikoti akiwa kwenye mpango ndani ya Azam FC na Simba.
Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery alisema kuwa ni ngumu kwake kuzungumza juu ya wachezaji wake kuondoka ila anatambua wanafanya kazi kwa juhudi.
“Wachezaji wangu wote wanajituma kutimiza majukumu yao hilo ninalitambua ila kuhusu kuondoka kwao kwa sasa bado siwezi kuzungumzia kwa kuwa ni wakati wa ligi na usajili haujafunguliwa,” alisema.