UONGOZI wa Gwambina FC umesema kuwa malengo makubwa ni kuona inashiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa kuwa imejipanga kuona inafikia malengo hayo.
Gwambina ipo nafasi ya kwanza kwenye kundi B ikiwa imecheza mechi 18, kibindoni ina pointi 40 ikiwaacha kwa pointi 10 walio nafasi ya pili Geita Gold.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mkuu wa Idara ya Mashindano wa Gwambina FC, Mohamed Moshi maarufu kama Mtabora amesema kuwa mipango ipo vizuri.
“Kila kitu kinakwenda sawa na tunaamini kwamba tutafikia malengo ya kushiiki Ligi Kuu Bara msimu ujao kwani ni jambo la kusubiri tu kwa sasa.
“Tumebakiwa na mechi nne ili kukamilisha mzunguko wa pili na tunahitaji pointi tatu ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki ligi, hilo linawezekana kikubwa sapoti,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.