Uncategorized

WATATU KIKOSI CHA KWANZA WA YANGA LEO KUIKOSA JKT TANZANIA

admin June 16, 2020 9:47 pm


LEO, Juni 17 Yanga itakuwa kazini ikimenyana na Klabu ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Itakosa huduma ya wachezaji wake watatu ambao ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Luc Eymael kutokana na sababu mbalimbali.

Papy Tshishimbi, nahodha wa Yanga bado hajawa  fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha, Lamine Moro beki tegemezi anasumbuliwa na maumivu ya mguu aliyapata kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC.

Kuanza kwake leo itategemea na maamuzi ya Eymael kwa kuwa amekuwa ni mhimili kwenye safu ya ulinzi.

Kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison bado hajajiunga na timu kwa kuwa bado yupo Dar hajaibuka Dodoma kwa kile alicheleza kuwa bado ana maumivu ya goti.

MKUDE SASA YUPO CHINI YA UANGALIZI MAALUMU ILI KUREJEA KWENYE UBORA WAKE DILI LA RUTANGA YANGA HAWA WAMEHUSIKA KUMPA MIAKA MIWILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply