LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amewaomba mashabiki wa masuala ya michezo kumsamehe beki wa Klabu hiyo, Lamine Moro kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichokifanya mbele ya nahodha wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto.
Moro alionekana akimpiga teke Kazimoto kwenye mchezo uliochezwa jana, Juni 17 Uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:00 jioni ambapo Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Eymael amesema:”Ni jambo baya kwa mchezaji kulifanya ila hakukusudia, nimeongea naye na yeye mwenyewe amekiri kuwa amefanya makosa, katika hali ya kawaida anahitaji msamaha kwani mpira wa miguu una kanuni zake na kile alichokifanya amejutia.
“Ombi langu pia wadau wa masuala ya michezo mumpe msamaha kijana ameomba msamaha nina amini hatarudia na wale wengine wenye tabia kama zake iwe somo wasifanye makosa yanaumiza,” amesema.
Moro amesema kuwa haikuwa dhamira yake ila ilitokea ghafla katika hali ya mchezo hivyo anahitaji msamaha.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.