Uncategorized

PICHA ZIMA LA JKT TANZANIA V YANGA LILIKUWA NAMNA HII

admin June 18, 2020 9:47 am

PATRICK Sibomana, mshambuliaji wa Yanga, jana alipindua meza kibabe kwa kufunga bao la kusawazisha mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mchezo huo ulikamilika kwaYanga kufungana na JKT Tanzania, bao 1-1 na kugawana pointi mojamoja, makao makuu ya nchi ya Tanzania, Dodoma.
Licha ya Michael Aidan wa JK Tanzania kufunga bao akiwa nje ya 18 kwa kuachia shuti kali dakika ya 13 halikuwapa pointi tatu JKT Tanzania.
Kuingia kwa Sibomana kulibadilisha mchezo jumla kwa kutuliza timu baada ya kunyanyuliwa benchi na Kocha Mkuu, Luc Eymael dakika ya 52 akichukua nafasi ya kiungo mshambuliaji Mapinduzi Balama.
Bao la Yanga lilipatikana baada ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima  kuachia shuti kali langoni mwa JKT Tanzania lililotemwa na mlinda mlango wa JKT Tanzania ndipo likakutana na guu la Sibomana aliyeujaza moja kwa moja langoni.
Ushindi huo unaifanya Yanga ikusanye jumla ya pointi nne kwa JKT Tanzania msimu huu na mabao manne kwani kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga ilishinda mabao 3-2.
 Beki Lamine Moro wa Yanga alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 88 kwa kumchezea mchezo usio wa kiuungwana Mwinyi Kazimoto wa JKT Tanzania ambaye naye pia alionyeshwa kadi nyekundu.
AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA BUSUNGU AFUNGUKIA USAJILI WAKE YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply