Uncategorized

DUH! KUMBE TEKNOLOJIA YA GOLI ILICHANGANYIKIWA NA BAO LILILOFUNGWA

admin June 19, 2020 5:47 am

IMEELEZWA kuwa refa wa mchezo uliopigwa Juni 17, kati ya Aston Villa anayokipiga nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta dhidi ya Sheffield United uliichanganya teknolojia ya goli pamoja na macho ya mwamuzi wa kati.

Kwenye mchezo huo Sheffield United ilipata bao kipindi cha kwanza ambalo liliokolewa na mlinda mlango wa Aston Villa Orjan Nyland ambaye aliingia nao ndani ya goli.

Taarifa zinaeleza kuwa kamera saba ndani ya uwanja zilishindwa kuelewa usawa wa mlinda mlango,mabeki wake pamoja na eneo la lango la goli huku ikielezwa pia hata mwamuzi wa kati alichanganyikiwa.

Michael Oliver aliyekuwa mwamuzi wa kati alitazama teknolojia ya goli haikumpa jibu sahihi jambo ambalo Sheffield United walilamikia suala hilo baada ya dakika 90 kukamilika kwa timu hizo kutoshana bila kufungana.

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA SAKATA LA MORRISON LIKIWA LIMETUA TFF, SIMBA WALIJIBU KIMTINDO NAMNA ISHU ILIVYO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply