Uncategorized

NAMUNGO YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

admin June 19, 2020 5:47 am

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Juni 20, Uwanja wa Majaliwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa amewaandaa wachezaji wake kisaikolojia baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union ya Tanga, Mkwakwani Juni 13.
“Wachezaji wangu nimewaandaa kisaikolojia baada ya kupata pointi moja mbele ya Coastal Union pale Mkwakwani, unajua ushindani kwa sasa ni mkubwa nasi tuna malengo yetu ambayo tumejiwekea,” amesema Thiery.
Namungo FC ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 51 inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya nane na pointi 41 zote zimecheza mechi 29.
SAKATA LA MORRISON LIKIWA LIMETUA TFF, SIMBA WALIJIBU KIMTINDO NAMNA ISHU ILIVYO KAZIMOTO NA LAMINE SASA MAMBO FRESH

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply