Home Uncategorized SINGIDA UNITED KULIAMSHA KESHO MBELE YA JKT TANZANIA

SINGIDA UNITED KULIAMSHA KESHO MBELE YA JKT TANZANIA


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kazi kubwa iliyobaki ndani ya Ligi Kuu Bara ni kushinda mechi zote ikiwa ni pamoja na mechi dhidi ya JKT Tanzania itakayochezwa kesho, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wapo kwenye hatari ya kushuka daraja ni lazima wapambane.
“Nafasi ambayo tupo kwa sasa sio nzuri, hilo lipo wazi lakini tuna chaguo moja tu la kufanya ili kubaki ndani ya ligi kwa kushinda mechi zote ambazo zimebaki.
“Zimabaki mechi tisa ambazo kwetu ni ngumu tunaamini tutapambana ili kupata matokeo kwenye mechi hizi ili tubaki ndani ya ligi, kazi ipo,” amesema Katemana.
Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 29. Kwenye mchezo wa kesho hakutakuwa na mashabiki baada ya Serikali kuzuia mashabiki baada ya JKT Tanzania kushindwa kufuata muongozo kwenye mechi waliyocheza Juni 17 dhidi ya Yanga.
SOMA NA HII  NCHIMBI ABADILI GIA YANGA