Uncategorized

HAWA HAPA WAKALI WA MIPIRA ILIYOKUFA NDANI YA YANGA NA AZAM FC

admin June 20, 2020 4:47 am
KESHO Uwanja wa Taifa patachimbika kwa mechi kali kati ya Yanga dhidi ya Azam FC ambayo ni ya Ligi Kuu Bara.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ambalo walijifunga wenyewe kupitia kwa beki wao Ally Mtoni,’Sonso’. 

Hawa hapa ni wakali wa kucheza na mipira iliyokufa ndani ya vikosi hivyo:-
Azam FC ina wakali watatu wa kutumia mipira iliyokufa.
Richard Djod ambaye kibindoni ana mabao manne alifunga bao moja kwa penalti.Agrey Morris ambaye ni nahodha ana bao moja ambalo alifunga kwa penalti pamoja na Nevere Tigere mwenye mabao matatu moja alifunga kwa faulo.
 Yanga wao mkali wao ni David Molinga ambaye amefunga mabao matatu kwa mipirailiyokufa. Amefunga kwa faulo mabao mawili na amefunga kwa penalti bao moja.
Patrick Sibomana ametupia bao moja alilofunga kwa mpira wa faulo ilikuwa mbele ya Ndanda FC kwa guu lake la kushoto.

Bernard Morrison ana bao moja alilowatungua Simba, Uwanja wa Taifa kwa faulo ndani ya ligi.
RASTA KUTOKA BURKINA FASO KUTUA YANGA,SIMBA DAKIKA 270 BINGWA,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI OLE GUNNAR SOLSKJAER AMTAJA POGBA KUWA MCHEZAJI BORA DUNIANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply