Uncategorized

JKT TANZANIA V SINGIDA UNITED TAMBO TUPU

admin June 20, 2020 11:47 am

UONGOZI wa Singida United umesema kuwa  kikosi chao kipo tayari kuanza kuonyesha uwezo wao mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, leo Juni 20 majira ya saa 10:00 jioni.


Singida United iliyo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 itamenyana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya saba na pointi zake 43.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wachezaji wapo tayari kupambania kikosi chao ambacho hakina mwendo mzuri ndani ya ligi.

“Hatupo vizuri lakini kwa sasa wachezaji wamemaua kujitoa na kupambana kwa ajili ya timu, nina amini kwamba tutaanza kuonyesha matumaini ya kubaki ndani ya ligi kwenye mchezo wetu wa leo dhidi ya JKT Tanzania, ” amesema.

Abdalah Mohamed,’Bares, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa sera ya JKT Tanzania ipo palepale kucheza mpira wa pasi na wa darasani hivyo wana amini watapata matokeo mbele ya wapinzani wao Singida United.
COASTAL UNION WANA JAMBO HILI LEO MKWAKWANI MKWARA WA NAMUNGO NA KAGERA SUGAR ACHA KABISA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply