Home Uncategorized KOCHA MBAO AANZA NA MKWARA WA KUTOSHA

KOCHA MBAO AANZA NA MKWARA WA KUTOSHA


KOCHA Mkuu wa Mbao FC, Felix Minziro amesema kuwa ana matumaini makubwa na wachezaji wake watapambana kubaki kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Minziro amepewa mikoba ya kuwa kocha ndani ya Mbao FC iliyo nafasi ya 19 kwenye msimamo na pointi 23 baada ya kucheza mechi 30.

Mchezo wake uliopita Mbao FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na Azam FC Uwanja wa Chamazi.

Minziro ambaye alipigwa chini Alliance FC amesema kuwa:”Nimeongea na wachezaji na nimeona kwamba wana morali kubwa ya kufanya vizuri nina matumaini tutakwenda nao sawa.

“Nafasi ambayo tupo kwa sasa sio nzuri ipo wazi ila tutapambana ili kuona namna gani kikosi kitakuwa imara,” amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA CHAMA NA LUIS KUIVAA YANGA LEO MAPINDUZI IPO HIVI