Uncategorized

KOCHA SIMBA AUKUBALI MUZIKI WA KICHUYA

admin June 20, 2020 5:29 pm

KOCHA wa viungo wa Simba, Adel Zrane, amekiri kuimarika kwa kiwango cha winga wa kikosi hicho, Shiza Ramadhani Kichuya, baada ya kukaa benchi kwa muda mrefu.

Kichuya alirejea Simba dirisha dogo akitokea nchini Misri lakini ilikuwa ngumu kupata namba katika kikosi hicho kutokana na ushindani uliopo.

Mchezaji huyo alitumia vizuri kipindi cha mapumziko ya tahadhari ya corona kuimarisha kiwango chake na mechi ya Jumapili alianza kikosi cha kwanza na kuonyesha uwezo mkubwa.

Akizungumza na  gazeti laDIMBA Jumatano, Zrane alisema Kichuya wa sasa ni tofauti na alivyokuja, kwani amekuwa na kasi na yupo fiti kipindi chote walichoanza mazoezi anafanya vizuri.

“Ni kweli Kichuya amerudi katika kiwango chake, amekuwa na kasi kubwa, tunatarajia kuwa kadri anavyocheza ndipo ataendelea kuwa vizuri zaidi,” alisema.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO NDANI YA LIGI KUU BARA LAMINE AIPA YANGA HASARA NYINGINE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply