Uncategorized

MWADUI YATUMA UJUMBE HUU KWA MNYAMA

admin June 20, 2020 10:47 am


GERALD Mdamu, mshambuliaji namba moja wa Mwadui FC amesema kuwa mchezo wa leo mbele ya Simba watapambana kupata matokeo chanya ili kujihakikishia nafasi ya kubaki kwenye ligi msimu ujao.

Mwadui FC itakaribishwa na Simba leo, Juni 20, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa kupoteza kwa mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga kunawapa hasira ya kutafuta matokeo mazuri mbele ya Simba.

“Tulipoteza mchezo wetu uliopita mbele ya Yanga hilo lipo wazi kwani tulishindwa kuwafunga lakini hiyo haina maana kwamba na leo tutafungwa hapana.

“Kila mmoja anatambua jukumu lake hivyo nina amini kwamba tutafanya kazi kwa umakini na kutimiza majukumu yetu kwa wakati mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Mdamu ametupia mabao matano na kutoa pasi tatu za mabao kati ya mabao 27 yaliyofungwa na timu yake iliyo nafasi ya 12.

SIMBA:HAKUNA TUNACHOKITAKA LEO ZAIDI YA USHINDI LIPULI IPO FITI KUWAVAA POLISI TANZANIA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply