UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa utapambana kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kushinda mechi zake nane ambazo zimebaki kwa sasa.
Mtibwa imecheza jumla ya mechi 30 kibindoni ina pointi 34, mchezo wake mbele ya Coastal Union, uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani ililazimisha sare ya bila kufungana.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wamejipanga kuona mechi zao zilizobaki wanashinda ili kujihakikishia nafasi ya kubaki kwenye ligi.
“Tupo nafasi mbaya kabisa huu ndio ukweli hatuwezi kuficha lakini kwa namna tulivyojipanga kwa mechi zetu zilizobaki tuna amini zitatupa matokeo mazuri na tutabaki kwenye ligi.
“Kazi ni moja kwa mechi zetu ambazo zimebaki kutafuta ushindi kwani hiyo ndio njia pekee ambayo itatufanya tubaki ndani ya ligi, hatupo tayari kufanya makosa kwa mechi ambazo zimebaki,” .