Uncategorized

MTUPIAJI NAMBA MOJA NDANI YA YANGA APEWA MKONO WA KWA HERI

admin June 23, 2020 11:47 am

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji namba moja ndani ya Klabu ya Yanga anatimka jumla msimu ujao baada ya kushindwa kuelewana na mabosi zake ambao ni Yanga.

Molinga ametupia jumla ya mabao nane ndani ya Yanga ambayo imecheza mechi 30 na kufunga mabao 33.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa hakuna mpango wa kumuongezea mkataba nyota huyo jambo ambalo linampa nafasi ya kutokuwepo ndani ya kikosi msimu ujao.

“Tayari safari yake imewadia na mkataba wake unaisha msimu unapokamilika hivyo hatakuwa ndani ya kikosi msimu ujao,” ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa sio wakati wa usajili hawezi kuzungumza kuhusu hilo. 

COASTAL UNION YAANZA KUZOEA MAZINGIRA YA MWANZA, LEO KUKIWASHA HASSAN KESSY KAMA KICHUYA TU MSIMBAZI..!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply