Uncategorized

KASEKE – HAIKUWA BAHATI MBAYA

admin June 24, 2020 6:00 pm

KUTOKANA na kuonyesha kiwango bora katika nafasi ya beki wa kulia, nyota wa Yanga, Deus Kaseke, amesema kuwa haikuwa bahati mbaya kwake kucheza eneo hilo kwani analimudu vizuri na ikitokea katakiwa kuendelea kulitumikia, atalitendea haki.

Kaseke ambaye amekuwa akicheza nafasi ya winga wa kulia, juzi kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Azam, kocha wake, Luc Eymael, alimtumia kama beki wa kulia nafasi ambayo huchezeshwa Juma Abduill.

Kaseke alipangwa kucheza eneo hilo baada ya Abdul kuwa nje ya uwanja akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika mechi zilizopita.

Katika mchezo huo wa juzi uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa suluhu, Kaseke alionekana kuimudu vizuri nafasi hiyo baada ya kutimiza majukumu yake ya msingi ya kukaba kiasi cha kutoonekana pengo la Abdul.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kaseke alisema: “Sio kama ni bahati mbaya nimepangwa vile, bali ni nafasi yangu sahihi ninayocheza, lakini tangu nije Yanga, nimekuwa natumika zaidi winga wa kulia.

“Hata kama kocha akipendezwa kuendelea kunitumia katika eneo hilo, nipo tayari kwa sababu najua naweza kulimudu vizuri.”

SVEN ATOA AHADI YA KARNE SIMBA…AWATAJA WACHEZAJI ..!!! VIDEO: BAO LA 12 LA MHILU MBELE YA AZAM FC LILIKUWA NAMNA HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply