Uncategorized

MARTIAL ASEPA NA MPIRA WAKE JUMLA WAKIIPA KICHAPO CHA MABAO 3-0 SHEFFIELD

admin June 25, 2020 6:47 am


ANTHONY Martial, nyota wa Manchester United jana alisepa na mpira wake baada ya kutupia mabao matatu mbele ya Sheffield United.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhaha kusaka pointi tatu.

Mabao hayo yalipachikwa dakika ya 7, 44 na 74 na kuwafanya wasepe na pointi zote tatu.

Ushindi huo unaifanya United kufikisha pointi 49 kibindoni ikiwa nafasi ya tano huku Sheffield ikiwa na pointi 44 nafasi ya nane zote zimecheza mechi 31.

Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Norwich City, Juni 27, inahaha kupata ushindi ili kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOIMALIZA MBEYA CITY, SASA INAHITAJI POINTI TATU KUBEBA UBINGWA BEKI YANGA AKUTANA NA RUNGU LA TFF, KAZIMOTO PIA NAYE YAMKUTA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply