Uncategorized

BIASHARA UNITED SASA KAZINI KESHO MBELE YA AZAM FC, BONGE MOJA YA MECHI

admin June 26, 2020 1:47 pm


AZAM FC, kesho ina kibarua cha kumenyana na Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Karume Mara.

Ikiwa chini ya Aristica Cioaba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.

Inakutana na Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza ambaye ametoka kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya KMC.

Kwenye mabao hayo manne, mshambuliaji wake Atupele Green alitupia mabao matatu na kusepa na mpira wake baada ya kufunga hat trick. Mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kupambana kufikia malengo yake.

Hesabu kubwa za Biashara United ni kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo huku Biashara United ikihitaji kumaliza ndani ya 10 bora.

Mchezo wao uliopita wa mzunguko wa kwanza, Biashara ilimalizwa kwa kutunguliwa mabao 2-1 jambo litakaloongeza ushindani hasa kwa kuwa Biashara Unted itakuwa kwenye utawala wake.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 huku Biashara United ikiwa nafasi ya tisa na pointi 43 zote zimecheza mechi 31.

WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI SIMBA KUOGELEA MAMILIONI KWA MTINDO HUU MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply