Uncategorized

MASHINE SABA ZA YANGA KUIKOSA NDANDA FC LEO TAIFA

admin June 26, 2020 10:47 pm


LEO Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu,  Luc Eymael itamenyana na Ndanda FC Uwanja wa Taifa mchezo wa Ligi Kuu Bara. 

Ndanda FC inanolewa na Kocha Mkuu, Meja Msataafu Abdul Mingange ambaye anaipambania timu isishuke Daraja ikiwa nafasi ya 15 Kwenye msimamo inakutana na Yanga iliyo nafasi ya tatu.

Mchezo wa Kwanza uliopigwa Nangwanda Sijaona, Yanga ilishinda bao 1-0 lililojazwa kimiani na Patrick Sibomana. 

Hawa hapa saba wataukosa mchezo wa leo :- 

Bernard Morrison anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi aliyopewa na Kamati ya Maadili mwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons. 

Papy Tshishimbi bado hajawa fiti.

Lamine Moro anatumikia adhabu ya kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Mwinyi Kazimoto Kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania. 

Ally Ally, Eric Kambamba,Andrew Vincent, Ramadhan Kabwili hawapo Kwenye mpango wa mwalimu

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI MSIMAMO WA KUNDI A LIGI DARAJA LA KWANZA UPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply