Uncategorized

MBAO YAJIPIGIA BAO 1-0 POLISI TANZANIA

admin June 28, 2020 4:47 pm


TIMU ya Mbao FC leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya wapinzani wake Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezawa Uwanja wa CCM Kirumba.

Wazir Junior mshambuliaji namba moja ndani ya Mbao FC alijaza kimiani bao hilo dakika ya 65 lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.

Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini imeyusha pointi tatu mazima leo mbele ya Mbao FC.

Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Mbao inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro ambaye alianza kushinda mbele ya Coastal Union bao 1-0.

Licha ya ushindi huo Mbao inabaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 32 na kujikusanyia pointi 29.

SASA MABINGWA SASA WA LIGI KUU TANZANIA BARA HUU HAPA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply