Uncategorized

MBELGIJI WA YANGA HATA HAMUELEWWI KWA SASA BERNARD MORRISON

admin July 1, 2020 1:47 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji, amesema kuwa haelewi kilichompata mchezaji wake Bernard Morrison kwani amekuwa akifanya mambo ambayo si ya kinidhamu.

Eymael amesema kuwa amejitahidi kutumia muda mwingi kuzungumza na nyota huyo ila bado anaona ana tabia nyingine ambazo anazijua mwenyewe jambo ambalo halimfurahishi.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na viongozi wa Yanga ambapo suala zima ni juu ya mkataba wake pale aliposema kuwa amesaini kwa muda wa miezi sita huku Yanga wakieleza kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili.

“Hakuna ninachokijua kuhusu Morrison kwa sasa kwani nimezungumza naye muda mrefu ila sielewi namna gani anaweza kuwa kwani amebadilika.

“Tatizo kubwa ni utomvu wa nidhamu amekuwa mwenye mabadiliko makubwa kwa sasa jambo ambalo linanifanya nisiwe na chaguo la kuongea juu yake.

“Masuala mengine itakuwa ni yeye na uongozi sitapenda kusema sana kuhusu hayo,” amesema.

Morrison hakuwa sehemu ya kikosi kilichopenya hatua ya robo fainali jana mbele ya Kagera Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

DStv YAJA NA DATE MY FAMILY, KESHO JULAI 2 KINAANZA RASMI JESHI LA SIMBA KUIVAA AZAM FC LIMEPANGWA SIKU HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply