Uncategorized

RASMI JULAI 12 TAIFA SIMBA KUKINUKISHA NA YANGA BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM FC

admin July 2, 2020 2:47 pm


BAADA ya Simba kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC,jana Julai Mosi, sasa rasmi itakutana na Yanga, Uwanja wa Taifa, Julai 12.

Simba itakutana na Yanga  iliyoshinda mabao 2-1 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa, Juni 30. 

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi za watani hawa wajadi kuamuliwa na dakika 90 na sio ubora wa kikosi.

Wakiwa wamekutana mara mbili kwenye mechi za Ligi Kuu Bara,  Simba haijapata ushindi mbele ya Yanga zaidi ya kuambulia sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa pili Simba ilinyooshwa bao 1-0 lililojazwa kimiani na Bernard Morrison kwenye dabi yake ya kwanza kwa kuwa alitua Bongo kwenye usajili wa dirisha dogo.

Hesabu kubwa za Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael ni kushinda mechi mbili ili kutwaa taji la Shirikisho litakalowapa tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

“Mechi zetu ambazo tunataka kucheza ni mbili nusu fainali na fainali, tukishinda zote tutatwaa taji inawezekana na tupo tayari,” amesema Eymael.

Sven Vandenbroec, Kocha Mkuu wa Simba hesabu zake ni kutwaa taji pia.

“Tumetwaa taji la Ligi Kuu Bara bado tunahitaji na la FA kwani ni mipango yetu tangu awali,” amesema. 

Mshindi wa mchezo wa nusu fainali atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Sahare All Stars dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

SportPesa YAIKABIDHI SIMBA ZAWADI YA HUNDI YA SHILINGI MILIONI 100 MUUAJI WA SIMBA AANZA KAZI LEO RASMI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply