Uncategorized

MUUAJI WA SIMBA AANZA KAZI LEO RASMI

admin July 2, 2020 6:47 pm


BERNARD Morrison leo ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa wa chuo cha Sheria, Dar es Salaam. 

Morrison alikuwa kwenye mvutano na uongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba wake jambo ambalo lilipelekea awe nje kwa muda.

Yeye alikuwa anasema kuwa ana mkataba wa miezi sita huku Yanga ikieleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili.

 Suala hilo lilitinga Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo alihojiwa jana na kutoa maelekezo yake.

Ameingia Kwenye rekodi za wageni waliofunga Kwenye dabi kwani aliwatungua bao 1-0 Simba walipokutana Uwanja wa Taifa, wanatarajiwa kumenyana Julai 12. 

RASMI JULAI 12 TAIFA SIMBA KUKINUKISHA NA YANGA BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM FC KESHO NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply