Habari za Michezo leo
Uncategorized

MSUVA APIGWA PINI NYINGINE NDANI YA EL JADIDA

admin July 3, 2020 1:47 pm


SIMON Msuva, winga wa kimataifa anayekipiga ndani ya Klabu ya Difaa El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco,’Botola Liague’ ameongeza dili la mwaka mmoja.

Thamani ya Msuva imeporomoka kutoka euro 700,000 (sh.bilioni 1.5) katika viwango vilivyotoka Desemba mwaka jana na mtandao wa Trasfermakt hadi kufikia euro 550,000 (sh.bilioni 1).

Viwango hivyo vimetoka Aprili 8 mwaka huu 2020.

Msuva alijiunga na Difaa El Jadida mwaka 2017 kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo umefikia tamati Desemba mwaka jana kabla ya kuongeza mkataba mpya.

Kwa mujibu wa Transfermakt, Msuva amesaini kandarasi ya mwaka mmoja unaotarajiwa kufika tamati Juni 30,2021.

HIVI NDIVYO AZAM FC ILIVYONYOOSHWA NA SIMBA DAKIKA 450 MWADUI FC YAZITAKA POINTI TATU ZA KMC KESHO, UHURU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply