Uncategorized

KAGERA SUGAR YASAHAU KUHUSU YANGA, HASIRA ZAO YAZIWEKA KWA RUVU SHOOTING

admin July 4, 2020 11:47 am

UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa unasahau masuala yote ya mchezo wao wa hatua ya robo fainali dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Taifa,Juni 30 kwa kufungwa mabao 2-1 hasira zao ni mbele ya Ruvu Shooting.
Kagera Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime ikiwa nafasi ya 8 na pointi 45,leo, Julai 4 inakutana na Ruvu Shooting iliyo chini ya Kocha Mkuu, Salum Mayanga Uwanja wa Kaitaba, ikiwa nafasi ya 11 na pointi 42 zote zimecheza mechi 32.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Maxime alisema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila lazima wapambane kupata matokeo kwani mfumo wa Kagera Sugar ni kutoa burudani.
“Mchezo wetu na Yanga tunaachana nao kwani matokeo hatuwezi kubadili na watanzania wanajua namna hali ilivyokuwa hivyo mipango yetu ni kuona tunapata matokeo mbele ya Ruvu Shooting,” alisema.
Leo itamkosa kiungo wake mwenye rasta kichwani, Awesu Awesu ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Yanga.


JAZBA UWANJANI WACHEZAJI TUZIPE KISOGO AFYA KWANZA ALIYEWAUA SIMBA TAIFA YUPO TAYARI KUWAVAA KWA MARA NYINGINE, ATOA AHADI KUBWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply