Uncategorized

SIMBA YATOA TAMKO LA KIBABE KUHUSU YANGA

admin July 4, 2020 6:47 am


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amesema kuwa alikuwa anataka akutane na Yanga, ndiyo sababu ya kuwafunga wapinzani wao.

Simba iliifunga Azam Julai Mosi, mabao 2-0 na kufanikiwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA ambapo watakipiga na Yanga, Julai 12, 2020.


Sven amesema kuwa kwenye mchezo wake uliopita wa ligi alipoteza hivyo atatumia muda wake mwingi kukinoa kikosi chake kupata matokeo chanya.

“Tulipoteza kutokana na kushindwa kuwa makini kwenye mchezo wetu wa ligi hiyo haitufanyi tuwe wanyonge kwa kuwa tunakutana nao basi tutajua namna itakavyokuwa.

“Uhitaji mkubwa ni kupata matokeo chanya ambayo yatatufikisha kwenye malengo yetu ya kutwaa taji la FA pia kama ambavyo tulikuwa tunahitaji taji la ligi,” amesema.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Juni 30.


MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI YANGA HAINA PRESHA NA SIMBA, MIPANGO YAO IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply