Uncategorized

MGUNDA ATAJA KILICHOIPONZA COASTAL UNION KUFUNGWA MBELE YA MBEYA CITY

admin July 7, 2020 11:47 am


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kupoteza kwa kufungwa mbele ya Mbeya City ni makosa ya wachezaji wake ndani ya uwanja.

Jana, Julai 6, Coastal Union ilikubali kichapo cha mabao 3-1 na kuacha pointi tatu zikienda na maji.

Mgunda amesema kuwa imekuwa ni mwendelezo wa makosa ya wachezaji wake kushindwa kutimiza kile anachowaambia jambo ambalo analibeba yeye kwa kuwa ndiye mwalimu.

“Makosa ni yaleyale ambayo wachezaji wanayarudia hivyo sina uwezo wa kufanya tukiwa kwenye mchezo zaidi ya kuangalia namna gani tunaweza kuweka usawa.

“Bado simuoni mtu wa kumlaumu kwa matokeo ambayo tunayapata lakini lazima tuyafanyie kazi ili kuwa na mwendelezo mzuri,” amesema Mgunda.

Coastal Union ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 33.

Kabla ya kucheza na Mbeya City ilitoka kupoteza mechi mbili kanda ya ziwa ambapo ilifungwa mbele ya Mbao FC na Alliance FC kote ilinyooshwa bao mojamoja.

SIMBA YAIPIGA MKWARA YANGA, HESABU ZAKE ZIPO NAMNA HII TFF YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA MORRISON KUDAI ALICHEZA MECHI MBILI BILA MKATABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply